JULIA DEDERER
MAREKANI
'Nina umri wa miaka 73, ninajishughulisha na mambo yanayonihusu kama nilivyokuwa nilipokuwa na umri wa miaka 30, labda hata zaidi. Sikuwahi kupata watoto. Nilihisi mvutano wa kijamii kuwa na watoto haswa katika miaka yangu ya 30, lakini, ukweli nimeona akina mama ambao wamekusudiwa kuwa mama na sikuwa na hiyo. Nimependa kuwa shangazi kwa watoto wa kaka zangu, kuwatazama wakikua, kuwa mtetezi wao kuweza kukua katika ubinafsi wao wa kujitegemea, kuwa kiongozi wao.
Ninajivunia chaguo ambazo nimefanya kuhusu taaluma yangu, kuhusu uhusiano wangu wa karibu na wanaume ambao nimewapenda. kuhusu sababu ambazo nimeweza kushiriki. Kwa hivyo nataka wanawake na wasichana wote wahisi uhuru wa kuchagua njia inayowafaa, sio kuhisi kushinikizwa na matarajio ya jamii.
Kwenye njia yoyote kuna matuta makubwa njiani. Ikiwa tunajua tunasafiri pamoja, ambayo sote tuko, TUNAWEZA kila mmoja wetu kulifuata!'